Blogs
Marketing tips
Marketing tips
Huwezi Kumshawishi Mtu Usiyemjua / Usiyemuelewa!
SOKO ndio Mzizi wa Kila kitu—na kila kitu kinaanzia Sokoni
WARNING: “Do not write a single word of copy until you understand the MINDSET of the person or persons who’ll read it.”
PS: Ignore those sacred words—and your copy will flop 99.9% of the time GUARANTEED!
SO:
Ndani ya “MARKET” (Soko) Tutaangalia Vitu Viwili:
Their Level of AWARENESS—(Kiwango chao cha Uelewa)
Their Identity PROFILE (Avatar)—(Wasifu wa Mlengwa/mteja)
Twende Tuanze Na:
AWARENESS Level
(Customer Bonding Quotient–CBQ)
Nilijifunza hii kutoka kwenye Kitabu cha “Eugene Schwartz” kinaitwa:
”Breakthrough Advertising”—($986)
PS:Hili ndilo Kaburi la 99% ya Copy sokoni—(Kwasababu wanapuuza kipengele hiki muhimu)
Kuna AWARENESS Level 5 za Wateja Sokoni:
1). Unaware
2). Problem Aware
3). Solution Aware
4). Product Aware
5). Most Aware
Kufanya UTAFITI
(a.k.a Research)
Nenda sehemu Wanazopatikana Hao watu kama:
Youtube—kuna videos nyingi zinazotangazo bidhaa/huduma youtube nenda kasome K,asome Comments utapata kila kitu
Facebook Groups, WhatsApp Groups, WhatsApp channels, Telegram Channels,
nk—Nenda kasome Comments za Malalamiko au Maoni
Amazon.com—Nenda kasome Reviews kwenye bidhaa husika utapata majibu kibao kuhusu bidhaa inayotibu changamoto kama yako
Online forums—Mfano Jamii forum kuna maoni kibao kule kuhusu bidhaa/huduma mbali mbali
Secret Weapon “Chat-GPT”—Hii ndio njia ya Haraka zaidi kuliko zote ya Kupata Kila kitu Unachohitaji kutoka kwa wateja wako ndani ya sekundo 60 tu kama utamlisha Chat-GPT Taarifa sahihi
…Kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho hapa ni Maswali sahihi ya kumuuliza—“Chat-GPT”
Jinsi Ya Kutumia ChatGPT Kufanya Utafiti wa Soko Lako ndani ya Sekunde 60 Tu
Miongoni mwa njia ya Haraka na uhakika zaidi ya kupata Taarifa zote kuhusu mteja wako ni Kutumia:
“Chat-GPT”
Na:
Hizi hapa chini ndio “FRAMEWORKS” za Kutumia:
Tuseme unataka Kujua “Vipingamizi” Vinavyomfanya Mteja Asinunue bidhaa/huduma yako
Utatumia Framework Ifuatayo Kumuuliza Swali— “ChatGPT”
[FRAMEWORK]
Mimi ni [Mfanyabiashara unayeuza nini na bidhaa yako ina faida gani na kwa nani?]. Nahitaji kujua ni Vikwazo/Vipingamizi gani [Mteja wako] Anaweza Kuvitumia kama Sababu ya Kutokununua bidhaa yangu?
Hatua # 1: Headline
Hatua # 2: Opening Hook
Hatua # 3: Establishing Credibility
Hatua # 4: Product Introduction/Reveal
Hatua # 5: Benefits
Hatua # 6: Price Appeal
Hatua # 7: Bonuses
Hatua # 8: Guarantee
Hatua # 9: FOMO/Urgency
Hatua # 10: Call to Action
Hatua # 11: Post-Script (PS)
Tuanze Na:
Hatua # 1: Headline
-Kazi ya Headline ni Moja Tu—Ku-Grab Attention ya Walengwa
-80% ya watu husoma Headline Tu
-Initial CAPS
-Bila Headline Tayari umeshapoteza 80% ya Pesa zako
Techniques Kuu 4 za Kuandika Headlines:
The How to Technique
The Dog Whistle Technique
Interest + Curiosity Technique
The Swiping Technique
The How to Technique
F1 : Jinsi Ya [Weka FAIDA ya Kile Unachokiuza]
Mfano unauza Herbal Cream:
-Jinsi ya kuwa na Ngozi Nyororo
U
-Jinsi ya kuwa na ngozi Nyororo ambayo Marafiki zako watakuonea Wivu
-Jinsi Ya Kuwa na Ngozi nyororo kama Hamisa Mobeto
F2 : Jinsi Ya (X) Ndani Ya (Y) Bila (Z)
X–Matokeo wanayoyataka
Y–Muda wa Kupata hayo Matokeo
Z–Vitu Wanavyovichukia
Mfano Unauza “Program ya Kupunguza Uzito”
-Jinsi ya Kupunguza 25Kg Ndani Ya Siku 15 Bila Kufanya Mazoezi /Kujinyima kula
The Dog Whistle Technique
Hapa unawaita walengwa moja kwa moja kwenye Headline yako—(a.k.a Call out your Audience)
Formula : Soma Hii Kama Unataka [Weka Matokeo Wanayoyataka]
Mfano:
-Soma Hii Kama Unataka Kuuza Bidhaa yako kwa Wateja 100 Kila Siku Mtandaoni
-Soma hii kama unataka Kujiajiri Ndani ya Siku 90 Zijazo
-Soma hii kama Unataka Kubeba Ujauzito Ndani ya Siku 30 Zijazo
Interest + Curiosity Technique
Interest—ni kile kitu ambacho wana Interest nacho/wanachokitaka
Curiosity—Kitu Kitakachowafanya Wadadisi au Washangae
Mfano 01:
Jinsi Mchanganyiko huu wa Almond na Aloe vera unavyoweza Kumfanya Mwanamke Yeyote Abebe Ujauzito Ndani ya Siku 29 Zijazo Guaranteed!
Interest–Kubeba Ujauzito
Curiosity–Almond na Aloe Vera
Mfano 02:
“Gundua Tiba Hii ya Nguvu za Kiume iliyokuwa inatumiwa Kisiri na Morani wa Kimasai Tangu Karne ya 17”
Interest–Nguvu za Kiume
Curiosity–Morani wa Kimasai
The Swiping Technique
Mbinu hii kwenye Music inaitwa “Sampling”
…ambapo sehemu ya nyimbo ya zamani (Hit song) inatumika kutengeneza nyimbo nyingine Mpya!
Mbinu hii kwenye kwenye Copywriting inaitwa “Swiping”
Unatafuta Headlines za Copy za Zamani zilizofanya Vizuri kisha una-Swipe Headline yako kutokea hapo
Mifano:
Headline hii iliandikwa na “Gary Bencivenga” alipokuwa anauza Kozi ya kujiandaa na Interview:
-Do You Make These Mistakes In Job Interviews?
Legendary Copywriter “Gary Halbert” aka-Swipe alipokuwa anauza Kozi ya Kuzungumza Kiingereza:
-Do You Make These Mistakes In English?
See More Headlines to Swipe from!
Hatua # 2: The Opening Hook
Hii ni ile sentensi ya kwanza baada ya Headline yako…
Na:
Kazi yake ni Moja Tu—Ku-HOLD Attention!
Njia Kuu 3 za Ku-Open Hook:
1. The question method
2. The promise method
3. The story method
The Question Method
Njii hii ni pale unapoanza sentensi yako kwa kuuliza swali linalolenga FAIDA ya kile unachokiuza…
(Hint: NLP)
Mfano 01:
Je ungependa kugundua Formula ya Siri ya Kukata Kitambi na Manyama Uzembe ndani ya Siku 21 Tu bila kujinyima kula wala Kufanya mazoezi?...
…kama umejibu Ndio–basi soma ujumbe huu mpaka mwisho–(Au Basi Ujumbe huu ni kwa ajili yako)
Mfano 02:
Je ungependa kunasa Ujauzito ndani ya siku 30 zijazo hata kama una hormone Imbalance?...
…kama umejibu Ndio–basi huu ndio ujumbe muhimu zaidi utakaousoma leo!
The Promise Method
Njia hii ni kinyume cha ile ya kwanza…
Badala ya kuuliza swali—hapa unampa Msomaji AHADI ya FAIDA atakayoipata endapo atasoma tangazo lako mpaka mwisho!
Mfano 01:
Mpendwa Mzazi…
Baada ya kusoma ujumbe huu mpaka mwisho utaenda kugundua Formula ya Siri ya kumfanya mtoto wako awe Genius na awepo kwenye Top 3 darasani kwake
Mfano 02:
Rafiki Mpendwa…
Utaenda kuacha Kazi ndani ya Siku 90 zijazo baada ya kusoma ujumbe huu mpaka mwisho endapo utafanya kila kitu nilichokuelekeza
The Story Method
Honestly hii ndio njia yenye nguvu zaidi kuliko zote—na hii ndio Silaha yangu ya Siri…
Kwanini?
Kwasababu Binadamu anapenda Stories na ubongo wa binadamu umetengenezwa kwa Stories
Tunaangalia Movies, tunasoma Vitabu vyote hivyo ni kwasababu tunahitaji kupata Stories
Changamoto pekee ya njia hii ni kwamba:
“Lazima Story iwe inavutia na inaendana na Kile kinachouzwa”
(Angalia Mifano wake kutoka kwenye My Swipe file)
Hatua # 3: Establishing Credibility
Hapa unatakiwa kuwapa Sababu ya Kwanini wanatakiwa kusoma Tangazo lako na kwanini Wakuamini...
Kuna Njia Kuu 3 za Kujenga Credbility Kwenye Copy yako:
Waambie kama una Utaalamu wowote ndani ya kile Unachokiuza—(Hapa unawapa CV yako)
Tumia Reviews za Wataalamu wengine ndani ya Niche husika kama Endorsement
(If you are selling poultry Food that makes chickens very big within a short period of time–you can seek the review of a professor in animal science at a university)
Weka SHUHUDA za wateja wako
Hatua # 4: Product Reveal
Hatua hii haina mbwembwe–tambulisha moja kwa moja kile unachokiuza…(Bidhaa/huduma yako)
Hatua # 5: Benefits
Hii ndio Hatua ya kuinadi na kuiuza bidhaa/huduma yako
[FORMULA: Features + Benefits]
(Use Bullets Points)
Tumia Haya Maneno Kuunganisha Kati ya Features & Benefits
“Kwahiyo/Hivyo Basi—(So That)”
Mfano:
Ina Camera (Meg Pixel 70)—Kwahiyo utaweza kupiga picha zenye Quality kubwa
Ina Internal memory Gb 128—Kwahiyo utaweza kuhifadhi vitu vingi kwa wakati mmoja….(hutoingia gharama ya kununua External/Memory Card)
Ina screen kubwa—Kwahiyo utaweza kuona vitu vyako kwa ukubwa zaidi ikiwemo videos & Picha
Betri yake inakaa na charge masaa 72—Kwahiyo utaweza kutumia kwa muda mrefu zaidi bila ku-charge
Hatua # 6: Price Appeal
Waambie bei ya bidhaa/huduma yako
Tahadhari: Usiweke bei moja kwa moja bila Kufanya Bargaining kwanza–ukifanya hivyo always itaonekana Expensive hata kama ni ndogo kiasi gani
“Price Vs Value”
Mfano:
Thamani ya “X” ni Tshs “Y” Lakini Kwasababu ya “Z” —Bai Leo utaweza kuipata “X” kwa malipo kidogo ya “Y” Tu
Thamani ya “The MCB” program ni Tshs 200,000 Lakini kwasababu hii ndio mara ya kwanza Program hii inaingia sokoni—basi leo utaipata The MCB Program kwa malipo kidogo ya Tshs 100,000 Tu
Hatua # 7: Bonuses
Weka Bonuses zinazoendana na kile unachokiuza–lengo ni kuongeza PERCEIVED Value
Kuna watu watanunua kwasababu tu ya Bonus Fulani
Attach Value kwenye kila Bonus
There are many kinds of Bonuses
Here are some that will give you ideas
● Free eBooks, audios, videos, etc
● Free software
● Free tutorials
● Free training
● Free consulting
● Free complimentary products
● Free membership
● Buy some get some free
● And lots more.
Hatua # 8 : Guarantee
Watolee RISK yoyote inayoweza kutokea endapo watanunua bidhaa/huduma yako kwa kuwapa Guarantee mojawapo kati ya hizi 3:
Money Back Guarantee—Ahadi ya kuwarudishia Pesa zao endapo hawatapata matokeo kusudiwa
Product Guarantee—Ahadi ya kuwabadilishia bidhaa nyingine endapo walionunua itakuwa na tatizo
Service Guarantee—Ahadi ya kuwafanyia FREE Service endapo Gari italeta shida…For Car Dealers
Hatua # 9 : Urgency (F.O.M.O)
Wape sababu ya kuchukua hatua Muda huo…
Watu hawawezi kuchukua hatua bila kuwawekea Hofu ya Kukosa
Kuna njia 2 za kuwafanya wachukue hatua Haraka:
Time Limit—(Ukomo wa Muda)
Mfano:
“Mwisho wa OFA Hii ni leo saa 11:59pm”
Quantity Limit—(Ukomo wa Idadi)
Mfano:
“OFA Hii ni Maalumu kwa watu 50 Tu”
Hatua # 10 : Call to Action (CTA)
Hapa hakuna mbwembwe…
Waambie tu nini cha kufanya ili wapate bidhaa/huduma yako
Hatua # 11 : Post-Script (PS)
Hii ndio hatua ya mwisho kabisa ya Copy yako!
“Hapa unaweka Taarifa za kuwakumbusha wateja wako jumla ya vitu watakavyopata kama watachukua hatua muda huo—pamoja na vitu watakavyokosa kama hawatachukua hatua muda huo”